Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha mapendekezo juu ya uanzishwaji kituo cha teknolojia ya tabia nchi

UM wakaribisha mapendekezo juu ya uanzishwaji kituo cha teknolojia ya tabia nchi

Umoja wa Mataifa umetangaza kuanza kupokea michango ya mawazo kwa ajili ya kuanzisha kituo maalumu cha teknolojia kitachohusika na masuala ya tabia nchi kama ilivyoagizwa na mkutano wa kimataifa uliofanyika mwaka uliopita huko Durban Afrika Kusini.

Kituo hicho pamoja na mtandao wake, pia kinatazamiwa kuchukua jukumu la kuendeleza mbinu mikakati ya kiteknolojia ambayo iliasisiwa kwenye mkutano mwingine wa kimataifa uliofanyika Cancun, Mexico mwaka 2010.

Imeelezwa kuwa mpango huo unashabaya ya kuongeza mashirikiano ya kiteknolojia pamoja na kukuza mashirikiano ya kimaendeleo hasa kwa nchi ambazo bado hazijapiga hatua kimaendeleo na zinakosa ushawishi wa kisayansi.

Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa iliyopewa jukumu la kuratibu mpango huo, imetoa mwito kwa mashirika mbalimbali pamoja na makundi mengine ya watu kuwasilisha mapendekezo yao kabla ya March 16 mwaka huu.