Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE kufanyia marekebisho sheria inayohusu magari makubwa

UNECE kufanyia marekebisho sheria inayohusu magari makubwa

Ikiwa na shabaha ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kwa nchi za Ulaya imeweka shabaha ya kufanyia marekebisho sheria ambayo inavibana baadhi ya vyombo vikubwa vya usafiri ambavyo vinahusika na utoaji kwa kiwango kikubwa hewa inayochafua mazingira.

Sheria hiyo ambayo inakusudia kuweka zingatia na viwango vipya kwa magari yanayotumia injini za kiwango cha juu inatazamiwa kuwasilishwa kwenye kongamano la kimataifa litakalofanyika mwezi June mwaka huu.

Hata hivyo marekebisho ya sheria hiyo yataanza kutumia rasmi kuanzia muhula wa kwanza wa mwaka 2013. Hatua hiyo inatizamwa kama jitihada za kukabiliana na vitendo vinavyochangia pakubwa uharibifu wa mazingira kwani inaelezwa kwamba moshi inatoka kwenye magari yanayotumia injini kubwa kubwa inachangia kwa kiwango kikubwa hali ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi.