Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu kulinda haki za binadamu barani Afrika wafanyika Ethiopia

Mkutano kuhusu kulinda haki za binadamu barani Afrika wafanyika Ethiopia

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na tume ya haki za binadamu ya Afrika imeandaa mkutano wa siku mbili kuhusu mipangilio na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kutafuta njia za kuboresha ushirikiano katika kulinda haki za binadamu barani Afrika.

Mkutano huo ulioandaliwa kati ya tarehe 18 na 19 mwezi huu mjini Addis Ababa nchini Ethiopia uliwaleta pamoja mashirika ya umma, Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wataalamu ni mmoja wa aina yake kuandaliwa.

Wataalamu hao walijadili kuchukua hatua za pamoja kama vile kutoa habari kwa pamoja, kutoa hamasisho za pamoja na kufanya ziara za pamoja barani Afrika.