Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutaendelea na vilio vya kuitisha haki:Ban

Kutaendelea na vilio vya kuitisha haki:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa akina mama na wanaume wanataka haki zao kuheshimiwa akiongeza kuwa wengine wanahatarisha maisha kufanya maandamano ya amani wakiitisha maisha mema ya siku za baadaye.

Akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Ban amesema kuwa hakuna kunyamazisha kilio cha kuitisha haki akiongeza kuwa jukumu lao ni kuukaribisha wakati ambao sheria itaheshimiwa kuanzia amani na usalama, kwa biashara na maendeleo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)