Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM warejelea wito wake wa kutaka kusitishwa ujenzi kwenye ukingo wa magharibi

UM warejelea wito wake wa kutaka kusitishwa ujenzi kwenye ukingo wa magharibi

Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa mataifa Valerie Amos kwa mara nyingine amezungumzia athari za hatua ya Israel ya kuendelea na ujenzi wa makao ya walowezi wa kiyahudi kwenye ukingo wa Magharibi akisema kuwa ujenzi huo ni kizuizi kwa maendeleo ya kiuchumi na kwa huduma muhimu kwa wapalestina.

Akiongea na waandishi wa habari Bi Amos pia amezunguzmzia eneo la C ikiwa ni asilimia 60 ya ukingo wa magharibi linalokaliwa na Israel. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)