Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua mshauri mpya wa mzozo wa Cambodia

Ban amteua mshauri mpya wa mzozo wa Cambodia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Bwana David Scheffer kuwa mshauri wake katika masuala yanayohusu Khymer Rouge. Bwana Scheffer anatajwa kuwa ni mtu mwenye uzewo na upeo mkubwa na anatazamia kutoa mchango mkubwa hasa wakati huu wa kesi inayohusu mzozo wa Cambodia.

Umoja wa Mataifa ulianzisha mahakama maalumu ECCC kwa ajili ya kushughulia vitendo vya uhalifu viloivyofanyika mnamo mwaka 1975 hadu 1979 wakati wa enzi za Khymer Rouge. Mtaalamu huyo anachukua mahala palipoachwa na Clint William ambaye muhula wake ulikoma tangu Septemba 30 mwaka jana.