Rais wa Baraza Kuu la UM atiwa moyo na hatua ya Bahrain kukubali kutekeleza mapendekezo ya mageuzi

19 Januari 2012

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema kuwa ametiwa moyo na tangazo lililotelewa na mamlaka ya Bahrain iliyoarifu juu ya utayari wa kuanza kutekeleza mageuzi yenye shabaha ya kukaribisha maridhiano mapya.

Rais huyo ameyasema hayo baada ya kuwa na mazungumzo na Mfalme Hamad bin Issa Al Khalifa. Amesema azima hiyo ni mwelekeo mpya ambao unachukua mkondo wenye manufaa kwa wote.

Mapema mwazi Novemba mwaka jana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliitaka serikali ya Bahrain kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na tume huru ambayo iliendesha uchunguzi wake juu ya matumizi ya mabaya yaliyoendeshwa na serikali dhidi ya raia.

Bahrain hivi sasa imesema kuwa inachukua hatua mpya ya utekelezaji wa mapendekezo ya tume hiyo ili kufungua sura mpya ya maridhiano

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter