Misaada zaidi yahitajika kuwasaidia waathiriwa wa mapigano nchini Sudan:Rice

Misaada zaidi yahitajika kuwasaidia waathiriwa wa mapigano nchini Sudan:Rice

Misaada inahitajika kwa dharura kwenye majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile ili kuzuia hali iliyopo sasa kabla ya hali ya njaa haijatangazwa. Mjumbe Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice alitoa onyo hili mda mfupi baada ya mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan. Rice anasema kuwa serikali ya Sudan imezuia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Umoja wa Mataifa na watoa huduma za kibinadamu kutoa huduma kwa watu walioathirika kwenye majimbo hayo mawili. Mzozo huu umewaathiri zaidi ya watu 500,000 na kama hawakutakuwa na misaada hadi mwezi machi mwaka huu hali huenda ikawa mbaya zaidi.