Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza kuandaa mkutano kuhusu Somalia mwezi ujao

Uingereza kuandaa mkutano kuhusu Somalia mwezi ujao

Mkutano kuhusu Somalia unatarajiwa kuandaliwa mjini London nchini Uingereza mwezi ujao. Mkutano huo uliotangazwa na waziri mkuu wa uingereza utawaleta pamoja wawakilishi kutoka karibu nchi arobaini kujadili kile jamii ya kimataifa inaweza kufanya ili kupata suluhu la mzozo uliopo nchini Somalia.

Miaka ishirini ya mapigano nchini Somalia imekuwa athari kubwa kwa watu wa Somalia nchi iliyoathiriwa pia na ukame. Uingerereza inakadiria kuwa kati ya watu 50,000 na 100,000 wameaga dunia nchini Somalia nusu yao wakiwa ni watoto tangu itangazwe njaa miezi sita iliyopita.