Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mmarekani Ertharin Cousin ateuliwa kuongoza WFP:FAO/Ban

Mmarekani Ertharin Cousin ateuliwa kuongoza WFP:FAO/Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva leo wametangaza uteuzi wa Bi Ertharin Cousin raia wa Marekani kuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP. Bi Cousin atachukua nafasi ya mkurugenzi mtendaji wa sasa Josette Sheeran.

Bodi ya wakurugenzi ya WFP imethibitisha kuafikia uteuzi huo. Ban na Da Silva wameelezea shukrani zao kwa Bi Sheeran kwa uongozi bora wa WFP katika miaka mitano aliyekuwa mamlakani na kuongeza kuwa amekuwa kinara wa kuchagiza masuala ya Umoja wa Mataifa na katika kuwasaidia watu masikini duniani na wale wasiojiweza. Hivi sasa ni mwakilishi wa Marekani FAO, aliwashawishi kufanya kazi katika utawala wa Rais Bill Clinton na ana ujuzi wa miaka 25 katika mashirika ya kitaifa na kimataifa na digrii na stashahada ya udhamili kutoka katika chuo kikuu cha Illinoi na chuo cha sheria cha Georgia.