Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majanga 302, yamekatili maisha 29,782, kuathiri watu milioni 206 na hasara ya dola milioni 366 2011:UM

Majanga 302, yamekatili maisha 29,782, kuathiri watu milioni 206 na hasara ya dola milioni 366 2011:UM

Kwa miaka miwili mfululizo majanga ya muda mrefu yaliyoambatana na matetemeko ya ardhi yamekatili maisha ya maelfu ya watu na kuathiri wengine mamilioni mwaka 2010 na 2011, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizochapishwa leo Jumatano na CRED na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na upunguzaji wa majanga UNISDR.

Kwa mujibu wa mkuu wa UNISDR Margareta Wahlstrom tetemeko lililoikumba Japan likiambatana na tsunami ni kumbusho kwamba hatuwezi kumudu kusahau funzo la kihistoria lililotokana na zahma hiyo.

Amesema mwaka 2010 watu zaidi ya 220,000 walikufa Haiti na tetemeko kubwa kuwahi kutokea katika miaka 200., na kuongeza kuwa maandalizi yasipofanyika ipasavyo basi dunia itashuhudia athari kubwa zaidi. Takwimu hizo zilizotolewa na CRED na UNISDR zinaonyesha kwamba watu 29,943 wamekufa katika matetemeko 2011 kati ya watu 29,782 waliokufa katika majanga 302. Idadi hiyo inajumuisha matetemeko ya Japan, Uturuki, New Zeland, na mafuriko ya Brazili, Thailand na Ufilipino, na kimbunga Marekani.