Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajibu wa kulinda umedhihirika bayana 2011:Ban

Wajibu wa kulinda umedhihirika bayana 2011:Ban

Mwaka 2011 historia ilipinduka na kuwa ya mafanikio. Wajibu wa kulinda ulidhihirika bayana, misingi yake kujaribiwa kuliko wakati mwingine wowote amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Akizungumza Jumatano kwenye mkutano wa Stanley Foundation hapa New York unaozungumzia wajibu wa kulinda. Ban amesema matokeo yake hayalingani lakini hatma yake maelfu ya maisha ya watu yameokolewa.

Amesema matumaini yamepatikana kwa watu ambao wamekandamizwa kwa muda mrefu akitolea mfano Libya, Ivory Coast, Sudan Kusini, Yemen na Syria na kuongeza kuwa kwa kali na hatua zilizochukuliwa na Umoja wa Maataifa zimedhihirisha kwamba kuwalinda binadamu ni dhumuni la Umoja wa Mataifa katika karne hii ya 21.

Ban pia amesema Umoja wa Mataifa umepata fundisho kwamba, hauwezi kusimama kando wakati unapopewa changamoto ya kuchukua hatua , ambapo kuna hatari ya wazi ni lazima hatua zichukuliwe lakini kwa umakini mkubwa.