Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2012 ni mwaka mwingine wa msukosuko wa kiuchumi:Benki ya Dunia

Mwaka 2012 ni mwaka mwingine wa msukosuko wa kiuchumi:Benki ya Dunia

Uchumi wa dunia mwaka huu wa 2012 unatarajiwa kukua kwa asilimia 2.5 tuu na hii ni kutokana na athari za matatizo ya kiuchumi yaliyoighuba dunia tangu mwaka 2008.

Takwimu hizi zimetokana na ripoti ya Bank ya dunia ya matarajio ya uchumi wa dunia kwa mwaka 2012 iliyotolewa leo Jumatano. Matatizo ya madeni barani Ulaya yaliyofurutu ada mwezi Agosti 2011 yanakwenda sambamba na kuzorota kwa ukuaji wa uchumi katika mataifa makubwa yanayoendelea kama Brazil, India na kwa kiasi fulani Urusi, Afrika ya Kusini na Uturki.

Na hasa kutokana na sera za mwishoni mwa mwaka 2010 na mwanzoni mwa 2011 za kukabiliana na shinikizo la ongezeko la kasi la mfumoko wa bei Andre Burns ni afisa wa Bank ya dunia.

(SAUTI YA ANDREW BURNS)