Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawatafutia makao watoto waliokimbia Libya

UNHCR yawatafutia makao watoto waliokimbia Libya

Jumla ya watoto 33 wasiokuwa na wazazi waliokimbilia Tunisia kutoka Libya watapewa makao nchini Norway kulingana na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Watoto hao ni kutoka nchini Somalia, Sudan, Ethiopia na Eritrea. UNHCR inasema kuwa idadi kubwa ya watoto hao waalikimbia taifa la Libya wakati wa mapigano yaliyoikumba nchi hiyo. Adrian Edwards kutoka UNHCR anasema kuwa watoto hao hawakuwa na wazazi walipowasili Libya na wengine walipoteleana na wazazi wao wakati wa kuhama kwa wahamiaji kutoka Libya.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)