Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Kipindupindu wazuka kaskazini mashariki mwa DRC

Ugonjwa wa Kipindupindu wazuka kaskazini mashariki mwa DRC

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umelikumba eneo la Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hasa mjini Bunia wilayani Ituri, Koga na Matete kwenye eneo la ziwa Albert.

Maeneo mengine yaliyoarifiwa kukabiliwa na ugonjwa huo ni maeneo ya Kivu ya Kusini mjini Bukavu. Serikali na mashirika ya wahisani katika maeneo hayo wanawahimiza raia kuhusu mbinu za kujikinga na ugonjwa huo ili usiweze kusambaa zaidi. Anjele Adronga ni kutoka moja ya mashirika yanayosaidia la Solidaritee Internasonale mjini Ituri

(SAUTI YA ANJELE ADRONGA)