Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi la dola 300 lazinduliwa kwa ukanda wa Gaza na ukingo wa Magharibi:UNRWA

Ombi la dola 300 lazinduliwa kwa ukanda wa Gaza na ukingo wa Magharibi:UNRWA

Miaka mitatu baada ya kumalizika kwa vita vya ukanda wa Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limetoa ombi la dharura la dola milioni 300 kwa ukada wa Gaza na ukingo wa Magharibi.

Akiongea kwenye ukanda wa Gaza naibu kamishina mkuu wa shirika hilo Margo Ellis amesema kuwa athari za kivita bado zinasalia na mahitaji kwa watu wa ukanda wa Gaza bado ni makubwa. Akiongea na waandishi wa habari Ellis amesema kuwa bado ukanda wa Gaza uko chini ya vizuizi huku wenyeji wake wakipitia mateso. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)