Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia kwenye hatari ya kuporomoka

Uchumi wa dunia kwenye hatari ya kuporomoka

 

Ripoti mbili za Umoja wa Mataifa hii leo zimeonya kuwa uchumi wa dunia uko kwenye hatari kuporomoka. Ripoti hizo zinasema kuwa huenda hali hiyo ikaziathiri zaidi nchi zilizostawi. Zinasema ripoti kuwa hatari iliyopo kwa sasa ni ya juu zikikadiria kuwa uchumi wa dunia utadorora kwa nusu asilimia mwaka 2012.

Ripoti kutoka kwa shirika biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD imesema kuwa ukuaji wa uchumi ulikuwa ni wa chini mwaka 2011 huku ikionyesha kuwa changamoto zinazoukumba uchumi wa dunia ni nyingi.