Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka El Salvador kuendeleza usawi wa kimaendeleo kwa wananchi wake

Ban aitaka El Salvador kuendeleza usawi wa kimaendeleo kwa wananchi wake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moom ameitaka El Salvador kuanza kushughulikia kero zinazokwamisha ustawi wa kijamii nchini humo na pia kuweka kipaumbele maeneo yanayohusu utawala wa kisheria.

Amesema nchi hiyo inawajibika kuondosha hali za kutokuwa na usawa ambazo zinanyima haki za kiuchumi na kijamii kwa makundi mengi ya watu. Ameongeza kuwa serikali ya El Salvador inapaswa sasa kuchapa kazi kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo na kuhakikisha inatoa matunda halisi kwa wananchi wake.

Amehitimisha kwa kusema kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la moja kwa moja la kuwajali na kuwaleta matumaini mapya watu wake hasa katika kipindi ambacho wananchi hao wanatarajia mema toka kwa serikali yao.