Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanza kufanya tathmini ya awali Ivory Coast

UM waanza kufanya tathmini ya awali Ivory Coast

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameanza kufanya tathmini ya awali nchini Ivory Coast ikiwa imepita miezi nane tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu ambao ulishuhudia kukiibuka hali ya uhasama na kuzua hali ya wasiwasi kwa miezi kadhaa.

Maafisa hao lakini wanaweka zingatio lao katika eneo linalohusu usambazwaji wa huduma za kiutu hasa katika maeneo ambayo yaliathiriwa vibaya na machafuko yaliyosababishw ana matokeo ya urasi.

Catheine Bragg ambaye anatoka katika ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya misaada ya kibinadamu OCHA, pamoja na kutembelea maeneo kadhaa ambayo hapo awali yaliripotiwa kuwa tete, lakini pia atatoa msaada wa kiutendaji kwa mamlaka za Ivory Coast.

Zingatio kubwa la ziara hiyo ni kutoa msukumo ambao utasaidia kurejea makwao kwa raia waliokimbia mtawanyiko kufuatia kuzuka kwa ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.