Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kolber ashutumu shambulizi la kigaidi lililotekelezwa nchini Iraq

Kolber ashutumu shambulizi la kigaidi lililotekelezwa nchini Iraq

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler ameshutumu vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya mauaji kwenye mji ulio kusini mwa Iraq wa Basra na kusababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi. Takriban watu 50 wanaripotiwa kuuawa kwenye shambulizi hilo lilitokea kwenye kituo cha ukaguzi kinachoelekea msikiti.

Kobler ametoa wito wa watu wote nchini Iraq kudumisha ushirikiano walio nao wakiwa na nia ya kumaliza ghasia na vitendo vya kigaidi. Ban pia alituma rambi rambi kwa familia za waliouawa kwenye shambulizi hilo na kuwatakia walio jeruhiwa nafuu ya haraka.