Ban apongeza maendeleo yanayopigwa na Tunisia tangu kujitokeza mapinduzi ya amani

16 Januari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban K-moon amepongeza mafanikio yaliyopigwa na nchi ya Tunisia tangu kujitokeza mapinduzi ya umma yaliyoundosha utawala wa rais wa nchi hiyo mapema mwaka jana.

Ban amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kutokea kwa mapinduzi hayo, Tunisia imeonya mfano kwa kupiga hatua kusonga mbele.

Katika taarifa yake akielezea hali ya mambo Tunisia, Ban ameongeza kusema kuwa macho ya masikio ya ulimwengu yalipelekwa moja kwa moja nchini humo kutokana na hatua waliyoichukua wananchi wan chi hiyo kubadilisha mfumo wa utawala.

Ameongeza kuwa wakati sasa mwaka mmoja umepita tangu kujitokeza kwa mapinduzi hayo, bado taifa hilo linasonga mbele katika hali ya ustawi na utengamao mkubwa.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter