Ban akitembelea kikosi cha UNIFIL nchini Lebanon

16 Januari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametembea kikosi kilichotwikwa jukumu la kuleta amani kusini mwa Lebanon akisisitiza umuhimu wa usalama wa vikosi vya umoja wa Mataifa vinavyohudumu kwenye maeneo hatari zaidi duniani.

Akiongea alipozuru eneo la Naqoura yaliyo makao makuu ya kikosi cha kudumisha amani nchini Lebanon cha UNIFIL, Ban aliitaja shughuli ya kuweka usalama nchini Lebanon kama hatari. UNIFIL imewapoteza wanajeshi 293 tangu ianze huduma zake nchini Lebanon mwaka 1978. Umoja wa Mataifa umepoteza idadi kubwa ya wanjeshi wanapohudumu na UNIFIL kuliko oparesheni yoyote ile ya Umoja wa Mataifa.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter