Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Liberia aahidi kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana

Rais wa Liberia aahidi kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana

Rais wa Liberia amesema kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na vita dhidi ya ufisadi ni ajenda anazozipa kipaumbele baada ya kuapishwa Jumatatu kuanza awamu ya pili ya utawala katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Rais Ellen Johnson Sirleaf ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na makamu wa Rais Joseph Boakai wamekula kiapo hicho mjini Monrovia na wataiongoza Liberia kwa kipindi kingine cha miaka sita.

Sherehe hizo za kuapishwa zimewaleta pamoja zaidi ya wageni 300 wakiwemo wakuu wa nchi, mawaziri wa mambo ya nje na mashirika ya kimataifa. Miongoni mwa wakuu wa nchi waliohudhuria ni kutoka Sierra Leone, Ghana, Rwanda, Senegal, Guinea, Benin, Namibia na Niger. Marekani imewakilishwa na ujumbe ulioongozwa na waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton.