Utalii wa kimataifa kufikia bilioni moja 2012:UNWTO

16 Januari 2012

Utalii wa kimataifa umekuwa kwa zaidi ya asilimia 4 kwa mwaka 2011 na kufikia watalii milioni 980 kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na shirika la kimataifa la utalii UNWTO. Wakati ukuaji ukitarajiwa kuendelea kukua mwaka huu wa 2012, katika kiwango cha polepole, watalii wa kimataifa wanatarajiwa kuvunja rekodi na kufikia bilioni moja baadaye mwaka huu.

UNWTO inasema utalii wa kimataifa mwaka 2011 umeongezeka ikilinganishwa milioni 939 wa mwaka 2010, licha ya kwamba mwaka ulighubikwa na matatizo ya uchumi, changamoto za kisiasa Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati na majanga ya asili kama Japan. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter