Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tisho la maradhi yasiyo ya kuambukiza ni kubwa kuliko unavyokadiriwa:WHO

Tisho la maradhi yasiyo ya kuambukiza ni kubwa kuliko unavyokadiriwa:WHO

Tishio litokanalo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa afya ya jamii duniani ni kubwa kuliko ilivyokadiriwa hapo kabla limesema shirika la afya duniani WHO. Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa WHO Margaret Chan ongezeko la unene wa kupindukia na uzito wa kupita kiasi ni onyo la ishara kwamba matatizo makubwa ya kiafya yanakuja.

Akizungumza katika mwanzo wa mkutano wa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo unaofanyika kila mwaka mjini Geneva Dr Chan amesema afya ya jamii ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijikita katika kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza sasa kuna haja ya kuelekeza nguvu zake kwa maradhi sugu yasiyo ya kuambukiza kama ya moyo na kisukari.

(SAUTI YA MARGARET CHAN)

Dr Chan ameongeza kuwa kushindwa kwa serikali kufadhili na kutekeleza sera zinazoweza kufanya kazi za afya ya jamii ni sababu kubwa ya kutokuwepo usawa na kuna uwezekano wa kuathiri usalama wa taifa na hata kupindua serikali.