Ni muhimu sasa kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala:Nassir

16 Januari 2012

Msisitizo umetolewa kuwa kuna haja ya haraka ya kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala leo hii kuliko wakati mwingine wowote. Watu zaidi ya bilioni moja wanaendelea kuishi bila kuwa na nishati ya umeme na kutimiza mahitaji ya muhimu ya kila siku amesema Rais wa Baraza Kuu Nassir Abdulaziz Al-Nasser.

Akizungumza kwenye mkutano wa tano wa dunia wa nishati mjini Abu Dhabi amesema suala la kupatikana kwa nishati ya kutosha na ya gharama nafuu halina mjadala na ni muhimu katika juhudi za kutokomeza umasikini, kuimarisha maisha ya watu, kupandisha viwango vya maisha na kufikia maendeleo endelevu.

Al-Nasser amesema wakati juhudi za kimataifa zikiendelea kukabiliana na changamoto za maendeleo ni muhimu ifahamike kwamba kutokuwa na nishati ya kutosha kuna athari katika usalama wa chakula, afya, usafiri, mawasiliano, maji na usafi.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter