Tunaweza kupiga hatua katika changamoto za nishati na mabadiliko ya hali ya hewa:Ban

16 Januari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za kuzalisha na kutumia nishati safi kwa wote akigusia faida zake kwa jamii na ukuaji wa uchumi duniani kote.

Akuhutubia mkutano wa shirika la kimataifa la nishati mbadala IRENA mjini Abu Dhabi Ban amesema ulimwengu unahitaji uongozi wa thabiti kufanikisha lengo hilo la kusambaza matumizi ya nishati mbadala.

Ban amesema wanachama wa IRENA wameusaidia ulimwengu kutambua kwamba nishati mbadala inaweza kupunguza gharama za uzalishaji viwandani na kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokana na nishati za jadi kama mafuta na makaa ya mawe.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban amesifu juhudi za IRENA za kubadili mfumo wa nishati na kusisitiza kwamba jitihada hizo zitasaidia katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa. Ban amebainisha kwa umeme tokanao na maji, upepo na teknolojia nyinginezo za nishati mbadala zaweza kuchangia katika kuboresha maisha na kongeza nafasi za kazi Afrika, Asia na kwengineko.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter