Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka wawekezaji kuwekeza kwenye maendeleo endelevu

Ban awataka wawekezaji kuwekeza kwenye maendeleo endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amewataka wawekezaji ulimwenguni kuanza kutupia jicho miradi inayozingatia maendeleo endelevu.

Amesema kuwa wawekezaji wanapaswa sasa kujitumbukiza kwenye masuala kama mabadiliko ya tabia nchi na kuanzisha fursa mpya ambazo zitaleta mbadala wa nishati sahihi kwa ulimwengu.

Katika ujumbe wake alioutoa kwenye kongamano la uwekezaji Mjini New York, Ban amesma kuwa katika zama hizi ambazo dunia inashuhudia mikiki mikiki kama ile ya mkwamo wa uchumi na hali ya fedha, sekta ya umma haiwezi kuzikabili changamoto hizo pekee.

Amesema nguvu ya wawekezaji binasfi na kwa kushirikiana na serikali na taasisi ulimwengu unaweza kufikia shabaha ya kuwa na majibu ya pamoja.

Pia amewakaribisha kujumuika kwenye kongamano kubwa linalotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambalo litajadilia umuhimu wa maendeleo endelevu.