Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bahrain bado imegawika

Bahrain bado imegawika

Nchi ya Baharain bado imegawika katika vipande vipande na wananchi wake wanaendelea kuisha katika mazingira ya hofu na wasiwasi mkubwa wa kuzuka machafuko na uvunjifu wa haki za binadamu.

Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu katika eneo la mashariki ya kati na nchi za kaskazini mwa afrika.

Frej Fenniche amesema kuwa hivi karibuni alipotembelea nchi hiyo alibaini kuwepo kwa hali ya wasiwasi na hofu miongoni mwa wananchi pamoja na taasisi za kiraia jambo ambalo linakwaza hatua za ustawi wa kijamii.

Bahrain ilionja joto la vuguvugu la maandamano ya amani kufuatia vugu vugu lilijitokeza katika nchi jirani ya Misri.