Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukosekana kwa usalama mpakani mwa Kenya na Somalia kunakwaza shughuli za usambazaji chakula-UNICEF

Kukosekana kwa usalama mpakani mwa Kenya na Somalia kunakwaza shughuli za usambazaji chakula-UNICEF

Kukosekana kwa usalama wa kutosha katika eneo la mpaka baina ya Somalia na Kenya kumezorotesha shughuli za upekekaji misaada ya kisamaria wema na hivyo kuzusha kitisho cha kuwepo utapiamlo.

 Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kitisho cha kukosekana usalama ndiyo kikwazo kikubwa kwenye eneo hilo.

Lakini eneo kama wilaya ya Turkana kiwango cha utapiamlo kimepungua kutoka asilimia 37 hadi kufikia asilimia 13.6 katika kipindi cha miezi sita iliyopita

 Hali hiyo imetokana na kuimarika kwa hali ya usalama ambayo imetoa msukuma kwa mashirika ya kutoa misaada kupenyeza huduma zake kwenye eneo hilo.

Maeneo mengine ambayo hali ya usalama inaidi kuzorota kumeshuhudiwa kiwango cha utapiamlo kikisalia katika alama za juu kabisa.