Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yafunga ofisi nchini Timor-Leste baada ya miaka 12 ya huduma

UNHCR yafunga ofisi nchini Timor-Leste baada ya miaka 12 ya huduma

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limefunga ofisi yake kwenye mji wa Dili nchini Timor-Leste baada ya kuhudumu nchini humo kwa muda wa miaka 12 ili kuwasaidia wakimbizi na watu wengine waliohama makwao. Sherehe za kufungwa wa ofisi hiyo zilifanyika kwenye ikulu ya rais.

UNHCR ilifungua ofisi hiyo mwezi Mei mwaka 1999 kufuatia ghasia za kura ya maoni baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Indonesia. Ghasia hizo zilizisababisha karibu watu 250,000 kukimbilia Timor Magharibi. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)