Waasi waendelea kuwavamia raia nchini DRC:OCHA

13 Januari 2012

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa kumekuwa na uvamizi wa raia kutoka kwa makundi yaliyojihami kwenye maeneo ya Shabunda, keleh na kabare mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo tangu Disemba 31 mwaka uliopita.

Uvamizi huo unaambatana na uchomaji wa nyumba , mauaji , ubakaji na uporaji wa mali. OCHA inasema kuwa watu 21 wamehamishwa kutoka mji wa Bukavu ili kupata matibabu zaidi huku wengine 4000 wakihama makwao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud