Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kambi za wakimbizi kwenye pembe ya Afrika hatarini:UNHCR

Kambi za wakimbizi kwenye pembe ya Afrika hatarini:UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linaelezea wasi wasi kutokana na ukosefu wa usalama nje na ndani mwa kambi zilizo makao kwa maelfu ya wakimbizi kwenye pembe ya Afrika. UNHCR inasema kuwa hali kwa sasa ni ya kutia hofu kwenye kambi ya Dadaab iliyo kaskazini mwa Kenya ambapo kuna tisho kubwa la kutokea kwa milipuko, utekaji nyara wa watu na magari na uhalifu mwingine. Viongozi wawili wakimbizi ambao walikuwa wamejitolea kudumisha amani na usalama kambini wakihudumu kwenye kambi za Hagadera na Ifo zilizo sehemu ya kambi ya Dadaab waliuawa hivi majuzi. Andrej (Tamka Andrei Mahechichi) Mahecic ni msemaji wa UNHCR.

CLIP