Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaboresha usafiri nchini Sudan Kusini

IOM yaboresha usafiri nchini Sudan Kusini

Shirika la kimatiafa la uhamiaji IOM linaboresha huduma za usafiri likitarajia kuhama kwa watu wanaokimbia mapigano nje na ndani mwa jimbo la Blue Nile na la Jonglei nchini Sudan Kusini. IOM imefungua ofisi ndogo kwenye mji wa Assosa ulio mji mkuu wa eneo la Benishangul Gumuz nchini Ethiopia na kuweka huduma za kuwasafirisha wakimbizi wanaovuka mpaka na kuingia kambini nchini Ethiopia.

Mabasi kumi pamoja na malori yamewekwa sehemu tofauti yanayoweza kusafiri kati ya umbali wa kilomita 60 na 200 ili kuwasafirisha wakimbizi hao. Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)