Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yasabisha uharibifu wa vituo vya afya Jonglei:WHO

Mapigano yasabisha uharibifu wa vituo vya afya Jonglei:WHO

Kufuatia makabiliano yanayoshuhudiwa kaskazini mwa Jonglei vituo vya afya mara huaribiwa na kufungwa. Kulingana na shirika na afya duniani WHO ni kuwa vituo vya afya vya Pibor pamoja na Lekuongole na Gumruk vilivyokuwa vikisimamiwa na shirika la Medecins Sans Frontieres pia viliharibiwa.

Wakati wa mapigano waathiriwa wengine na wanaohitaji huduma za kiafya hawakuwa na uwezo wa kufika vituoni kutokana na kuzorota kwa usalama. Wafanyikazi waliokuwa wakitoa huduma kwenye sehemu zilizoathirika walikimbia pamoja na wenyeji anavyoeleza Tarik Jasarevichi kutoka WHO.

(SAUTI YA TARIK JASAREVICHI)