Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC yasimamisha usambazaji wa misaada nchini Somalia

ICRC yasimamisha usambazaji wa misaada nchini Somalia

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC imesimamisha kwa muda usambazaji wa misaada iliyolenga kuwafikia watu milioni 1.1 baada ya bidhaa zake kuzuiwa kati kati na kusini mwa Somalia. Mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Somalia Patrick Vial anasema kuwa kusimamishwa huku kutaendelea hadi pale wale wanaoyadhibiti maeneo hayo watawahakikishia kuwa usambazaji wa misaada utaendelea na kuwafikia wanaoihitaji.

ICRC ni kati ya mashirika machache ambayo yakekuwa yakitoa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo hayo nchini Somalia. Usambazaji huu ulioanza mwezi Oktoba mwaka uliopita hadi sasa umewanufaisha watu milioni 1.1.