Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa haki za binadamu atumai kutokea mabadiliko Korea Kaskazini

Mtaalamu wa haki za binadamu atumai kutokea mabadiliko Korea Kaskazini

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK Marzuki Darusman ameelezea matumaini yake kwa nchi hiyo alipotangaza kuzuru kikazi Japan kuanzia tarehe 16 hadi 20 mwezi huu.

Mtaalamu huyo wa haki za binadamu amewasilisha maombi kadhaa ya kuzuru DPRK lakini hadi sasa hakuna lililofanikiwa. Amesema anatumai kuwa mabadiliko ya karibuni ya uongozi nchini humo kuchagiza mabadiliko ya sera ikiwemo sera zinazoathiri haki za binadamu za watu wa DPRK na zile zinazoathiri jirani zao kama Japan, na Korea Kusini.

Akiwa Japan mwakilishi huyo atakutana na viongozi wa serikali, makundi ya jumuiya za kijamii, mabalozi, familia za waliotekwa na waliojitenga na DPRK ambao kwa sasa wanaishi uhamishoni Japan.