Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama limetaka kuwe na msaada unaotolewa kwa wakati kwa AMISOM

Baraza la Usalama limetaka kuwe na msaada unaotolewa kwa wakati kwa AMISOM

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamesisitiza umuhimu wa kutolewa kwa msaada wa uhakika, unatostahili na kwa wakati muafaka kwa vikosi vya kulinda amani vya muungano wa Afrika AMISOM na wameitaka jumuiya ya kimataifa kuisaidia AMISOM kuimarisha uwezo wake ili kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Wazitaka pia taasisi zote za serikali ya mpito ya Somalia kushikamana, kuonyesha ari ya kisiasa na kujikita katika kutekeleza mpango wa amani walioafiki na kumaliza kipindi cha mpito ifikapo mwezi Agosti mwaka huu. Waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya Kusini Maite Nkoana Mashabane ambaye ni Rais wa baraza la usalama kwa mwezi huu amesema kuna fursa ya kuweza kutimiza muda huo wa mwisho.

(SAUTI YA MAITE MASHABANE)