Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka miwili baada ya tetemeko Haiti bado inahitaji msaada:Ban

Miaka miwili baada ya tetemeko Haiti bado inahitaji msaada:Ban

 

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka miwili tangu kutokea kwa tetemeko kubwa kabisa lililokikumba kisiwa cha Haiti Januari 12 mwaka 2010 Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa amesema ni fursa ya kuwaenzi watu zaidi ya laki mbili waliopoteza maisha yao katika zahma hiyo wakiwemo wafanyakazi 102 wa Umoja wa Mataifa.

Ban amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu tetemeko hilo katika kusambaza kifuusi na kuwapa makazi mapya maelfu ya watu waliopoteza kila kitu katika tetemeko hilo, Wahaiti wengi bado wanahitaji msaada wa kimataifa.

Katibu Mkuu kwa hivyo ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kulisaidia taifa la Haiti kwani ni muhimu sana kwa mustakhbali wa nchi hiyo. Hafla maalumu za kumbukumbu hii zimefanyika kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa Haiti MINSTAH.