Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yaitaka Baraza la Usalama kutoa msaada zaidi katika suala la Somalia

Kenya yaitaka Baraza la Usalama kutoa msaada zaidi katika suala la Somalia

 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alasiri ya leo linakutana kujadili hali ya Somalia. Somalia ambayo imekuwa bila serikali maalumu kwa zaidi ya miongo miwili sasa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo vita, ugaidi unaofanywa na wanamgambo wa Kiislam, ukame na tatizo la wakimbizi wa ndani na nje.

Kenya ambayo inahifadhi kundi kubwa la wakimbizi wa Somalia inasema ili kuweza kuwa na amani ya kudumu Somalia na kutoa afueni pia kwa pembe nzima ya Afrika msaada zaidi wa Umoja wa Mataifa unahitajika. Moses Wetangula ni waziri wa mambo ya nje wa Kenya yuko hapa New York kuhudhuria kikao hicho cha Baraza la Usalama anafafanua ajenda za mjadala wao.

(SAUTI YA MOSES WETANGULA)