Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wasiwasi bado inaikumba kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya

Hali ya wasiwasi bado inaikumba kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya

Wakimbizi wa Kisomali wanaoishi kwenye kambi ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya ya Dadaab wanaishi kwa wasiwasi, umesema Umoja wa Mataifa. Kambi hiyo inahifadhi zaidi ya wakimbizi 460,000 wengi wakiwa ni Wasomali waliokimbia machafuko na ukame nchini mwao.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasaidia masuala ya usalama kambini hapo kufuatia mashambulizi dhidi ya viongozi wa wakimbizi. Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR nchini Kenya Emmanuel Nyabera licha ya ulinzi wakimbizi bado wana hofu kubwa.

(SAUTI YA EMMANUEL NYABERA)