Maendeleo ndio ajenda ya mazungumzo kati ya Ban na waziri wa Nigeria

11 Januari 2012

Hali iliyojitokeza hivi karibuni nchini Nigeria ikiwemo hatua zilizopigwa katika uchunguzi wa mashambulizi ya bomu kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Abuja mwaka jana ni masuala yaliyopewa uzito katika mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Ulughenga Ayodeji Ashiru.

Watu 25 wakiwemo wafanyakazi 13 wa Umoja wa Mataifa walikufa kwenye shambulio la kigaidi lililofanyika tarehe 26 Agosti mwaka jana. George Njogopa na ripoti kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud