Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri yaanzisha majadiliano na nchi zinazotumia maji ya mto Nile:

Misri yaanzisha majadiliano na nchi zinazotumia maji ya mto Nile:

Tanzania na Misri zimeanza upya majadiliano yanayotaka kuwepo kwa suluhu ya kudumu kuhusu matumizi sahihi ya maji ya Mto Nile, huku kukiwa na shabaha nyingine ya kuzileta pamoja nchi zote zinazopitiwa na mto huo kwa ajili ya kuwa na majadiliano zaidi.

Majadiliano hayo yanakuja wakati ambapo nchini Misri ikiwa na utawala mpya, ambao unaanzisha juhudi za kulinda na kuvutia rasilimali zake, baada ya harakati kama hizo kushindwa wakati wa utawala wa rais Hosni Mubarak.

Nchi ambazo zimepitiwa na maji ya mto huo zipatazo saba, miaka michache iliyopita zilianzisha mkataba mpya unaotaka kuwepo kwa uwiano sawa wa matumizi ya maji ya mto Nile.

Waziri wa mambo ya Nje wa Misri Mohamed Kamel Amr hivi sasa ameanza safari ya kuzitembelea nchi hizo saba kwa ajili ya kuweka ushawishi kabla mkutano wao wiki ijayo Nairobi Kenya.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bwana Bernard Membe, kuna uwezekano sasa pande hizo zikafikia makubaliano yatayozingatia maslahi ya pande zote.

(SAUTI YA BERNAD MEMBE)