Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yameathiri utendaji wa serikali Yemen:UM

Machafuko yameathiri utendaji wa serikali Yemen:UM

Machafuko ya karibu mwaka mmoja yameathiri utendaji wa serikali na kulazimu mashirika ya misaada kufanyakazi na kushirikiana kwa karibu na wadau wa ngazi ya jamii na wafanyakazi wa kujitolea amesema afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Geert Cappelaere mwakilishi wa UNICEF Yemen amesema jukumu la serikali la kugawanya rasilimali , kusimamia utendaji na kufuatilia shughuli umepewa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake umedhoofishwa sana na hali ya machafuko.

UNICEF inasema sehemu kubwa ya Mashariki ya Kati wafanyakazi wa misaada wamekuwa wakilalamikia changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao huku machafuko ya kisiasa na maandamano ya kupinga serikali yaliyoghubika ukanda huo mwaka jana yamesababisha hali kuwa mbaya zaidi.

Misri kwa mfano mawaziri wanabadilishwa kila baada ya wiki kadhaa na Libya serikali ya mpito imekwa ikisita kuchukua hatua za kushughulikia masuala kadhaa ya muhimu.