Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu na G77 kuongeza mara mbili juhudi za kuendelea ajenda za maendeleo za UM

Baraza Kuu na G77 kuongeza mara mbili juhudi za kuendelea ajenda za maendeleo za UM

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limesema litaendelea kuliunga mkono kudi la G-77 na hususani haja ya kuongeza mara mbili juhudi za kushughulikia changamoto na vikwazo vya ajenda za maendeleo za Umoja wa Mataifa. Kauli hiyo imetolewa na Rais wa baraza hilo Nassir Abdulaziz Al Nasser. Rais huyo amesema kwa pamoja G-77 na bara kuu ni lazima wahakikishe kwamba mipango na programu zilizoanzishwa kushughulikia mahitaji ya nchi zinazoendelea inapewa rasilimali zinazotakiwa.

Amesema na kwa kuwa siku zinajongea haraka za kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ni muhimu kwa vyombo hivyo viwili kufanya kazi pamoja kuhakikisha mchakato wa kufikia malengo hayo na kuimarisha uchumi na maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa.