Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aipongeza ANC kwa kutomeza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini

Ban aipongeza ANC kwa kutomeza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akisherekea siku ya kuzaliwa kwa chama tawala nchini Afrika Kusin African National Party ANC, amepongeza mchango mkubwa uliotolewa na chama hicho wakati wa kutokomeza utawala kibaguzi wa rangi lakini amekipa shime kuendelea kukaza mkwiji kupigania uhuru wa kweli, haki na kutokomeza kabisa mizizi yote ya ubaguzi wa rangi.

Katika risala yake kwa chama hicho, Ban amesema kuwa ANC ni zaidi ya chama cha kisiasa kwani kimefaulu kufufua matumaini mapya na kisha kuwaleta pamoja watu wa rangi zote.

Amesema kuwa viongozi wa chama hicho walibeba moyo wa kizalendo na kishujaa kwa kuendesha harakati ambazo baadaye ziliwakomboa wananchi wa taifa hilo na kuleta mustakabala mpya.

Pia amesifu na kupongeza mchango mkubwa ulioletwa na chama hicho ambao ametaka uendelezwa kwa maslahi ya watu wa eneo hilo.