Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Afrika zaafiki kushirikiana na UM kumkabili kiongozi wa LRA Kony

Nchi za Afrika zaafiki kushirikiana na UM kumkabili kiongozi wa LRA Kony

Nchi kadhaa za Afrika zimekubaliana kushirikiana na Umoja wa Mataifa ili kuongeza mbinyo wa kumsaka kiongozi wa kundi la Lord Restistance Army Joseph Kony pamoja na wafuasi wake.

Makubaliano hayo yamefikiwa Mjini Kishansa, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo wakati viongozi wa pande zote mbili walipokutana kwa ajili ya kuweka shabaha ya pamoja ya kuzikabili hujuma za kiongozi huyo.

Nchi hizo, zimekubali kuongeza mashirikiano ya karibu ili kufanikisha kampeni za kuleta kwenye ukomu usumbufu wa kiongozi huyo. Katika taarifa yake baada ya kumalizika kwa mkutano huo, vikosi vya Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo, vimesema kuwa nchi zote nne, DRC, Jamhuri ya Kati, Sudan Kusini na Uganda zimekubaliana kuruhusu vikosi vya kila nchi kuvuka mipaka ili kuongeza uwigo wa kumsaka Kony.