Miaka miwili baada ya tetemeko Haiti mamilioni bado wanakabiliwa na adha

10 Januari 2012

Miaka miwili baada ya tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti taifa hilo bado linakabiliwa na mahitaji makubwa ya kibinadamu, na watu takribani 520,000 wanaendelea kuishi katika makambi. Kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, na shirika la mpango wa chakula duniani WFP maradhi ya kipindupindu yamekatili maisha ya watu 7000 na hali ya usalama wa chakula imeathiri zaidi ya asilimia 45 ya watu kisiwani humo.

WFP inaendelea kusaidia miradi ya lishe ambapo watoto 110,000 wa chini ya umri wa miaka 5 na wanawake 65,000 wajawazito na wanaonyonyesha wanapata lishe.

Nalo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema linaendelea kusaidia serikali ya Haiti kupunguza idadi ya watu wanaoishi kwenye mahema mijini huku likiweka msingi wa ajira na ujenzi mpya wa taifa hilo. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud