Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango ya dharura kuwasaidia Wasudan Kusini inakamilishwa:OCHA

Mipango ya dharura kuwasaidia Wasudan Kusini inakamilishwa:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kiratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema mipango ya haraka ya dharura kukidhi mahitaji ya maeneo yaliyoathirika na machafuko Sudan Kusini inakamilishwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa misaada na itaanza kutekelezwa katika siku chache zijazo.

Kwa mujibu wa OCHA msaada wa chakula na bidhaa zisizo chakula inagawanywa hivi sasa kwa waathirika. Shirika hilo limeongeza kuwa operesheni ya msaada wa dharura Sudan Kusini itakuwa ngumu na ya gharama kubwa tangu kutiwa saini makubaliano ya amani mwaka 2005.

Washirika wa masuala ya misaada wanakadiria kuwa watu 60,000 wameathirika na machafuko ya karibuni. Msemaji wa OCHA Elizabeth Byrs anafafanua.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)