UNICEF yatoa ripoti baada ya miaka 2 ya tetemeko la ardhi Haiti

9 Januari 2012

Katika ripoti yake mpya tangu kupita kipindi cha miaka miliwi wakati taifa la Haiti liliposhambuliwa na tetemeko kubwa la ardhi, Shirika la Umoja a Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa hali jumla ya watoto bado siyo ya kuridhisha.

Kwenye ripoti yake hiyo UNICEF imesema kuwa hata hivyo kuna hali ya kuimarika kwa ustawi watoto licha kwamba kunasalia taaba za hapa na pale.

Kulingana na ripoti hiyo   kunajitokeza matumaini kaisi kwa baadhi ya maeneo ambayo yanaonyesha kuimarika hasa katika maeneo ya elimu, afya, lishe pamoja na ulinzi.

Tangu kujitokeza kwa mafutiko hayo , UNICEF imejishughulisha kwa kaisi kikubwa kuimarisha mifumo na hali jumla za watoto na imefaulu kuwasaidia zaidi ya watoto 750,000 kurejea shuleni.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud